Valentine Day imetokana na Mtakatifu, Mchungaji/Askofu wa Kanisa katoliki wa miaka ya 496 baada ya Kristo ambaye aliitwa Valentine.
Wengine wanamtaja kama Askofu wa kiprotestanti wakati wengine wakimtaja kama a Mtakatifu Padre/Askofu wa Kikatoliki ambao kwa pamoja wana historia iliyofanana.
Hata ndani ya Katoliki bado kulikuwa na kutofautiana kwa kumfananisha na kuhani wa huko Roma na askofu wa Temin na wa tatu ni Mchungaji wa Kiprotestanti ambaye taarifa zake hazijulikani ila inaaminika aliishia Afrika katika utumishi wake.
Katika kipindi hicho Papa Gelasius alidhamiria kumuenzi Valentine kwa kuweka siku ya 14 Februari kama siku ya wapendanao duniani.
Historia inaeleza kuwa Askofu Valentine alikuwa akifundisha na kufungisha ndoa za siri kwa vijana wadogo wapendanao ambao walipigwa marufuku kuoana katika sheria za kirumi wakati huo kwa sababu walikuwa bado ni wadogo.
Kwa sababu Valentine alikirimiwa na Mwenyezi Mungu karama za uponyaji, afisa mmoja wa magereza ambaye binti yake alikuwa ni kipofu aliposikia uwezo uliwekwa kwa Askofu Valentine ya uponyaji, alimwendea na kumuomba amponye binti yake apate kuona tena. Valentine alifanya hivyo kwa nguvu za Kimungu na binti huyo akapona na tangu hapo binti wa afisa wa magereza alimpenda Askofu Valentine na wakawa marafiki wa karibu.
Dola ya kirumi iligundua kuwa Valentine alikuwa akifundisha na kufungisha ndoa kwa vijana ambao bado ni wadogo kinyume na sheria za kirumi ambayo ilikataza vijana wadogo kuoa au kuolewa mpaka wakue wakubwa, dola ya kirumi ilimkamata na kumweka ndani mpaka hukumu yake itolewe.
Alihukumiwa kifo baadaye na muda mfupi kabla ya hukumu ya kifo kutekelezwa alimuomba kalamu na karatasi afisa wa magereza na kuandika barua ya kuagana kwenda kwa binti wa afisa wa magereza, maandishi ambayo yanaishi mpaka leo. Barua hiyo ndio inaaminika kuwa kadi ya kwanza ya valentine.
Baadaye valentine mwingine alitokea akampenda binti wa afisa wa magereza lakini maelezo yake haikupewa umuhimu na wanahistoria. Kwa hiyo tarehe 14 Februari kila mwaka ikawa ni siku ya wapendanao duniani.
Lakini siku hii ilikuja kuwekwa rasmi kuanzia karne ya 14.
Siku ya valentine ilikuwa kwa umaarufu na ukubwa na katika miaka ya hivi karibuni iligeuka na kuwa ya kibiashara zaidi kwa kuuza kadi nyingi za valentine.
Ukweli Kuhusu Siku Valentine, Tarehe 14 Februari
- Zaidi ya kadi milioni 1 sawa na 25% ya kadi zote huuzwa nchini Marekani tu.
- Siku ya valentine ni ya pili kwa ukubwa na umaarufu baada ya Krismasi
- Siku ya valentine huazimishwa kila mwaka tarehe 14, Februari
- Inakadiriwa kuwa zaidi ya kadi za valentine milioni 50 huuzwa duniani kote
- Kadi za valentine kwa umuhimu: huuzwa zaidi kwa waalimu, watoto, wamama, wake, na wapendanao
Alama Mbalimbali za Kadi ya Valentine na Maana Zake
Malaika mdogo — huyu malaika mdogo kwa kingereza anaitwa Cupid ambaye ina asili and utamaduni katika dola ya rumi na ikiwa na maana ya mungu wa upendo. Inaaminika kuwa, yeyote aliyechomwa na huyu malaika (mungu wa upendo) hatakufa bali ataangukia katika mapenzi
Ua waridi — Waridi ni ua maarufu duniani kwa kupeana nyakati za sikukuu na yenye alama ya uzuri.
Ua waridi huja na rangi mbalimbali na zote zikiwa na maana tofauti.
- Nyekundu: ni upendo au mapenzi,
- Manjano: kwa ajili ya urafiki na uwazi,
- Nyeupe: ikiwa na maana ya pendo la kweli na uwazi,
- Pinki: ni rangi ya urafiki na wapendanao,
- Nyeusi: inamaanisha kuagana kwa wapendanao
Zawadi Zinazotolewa pamoja na Kadi ya Valentine
Angalia hapa chini baadhi ya zawadi zinazotumwa pamoja na kadi ya valentine
Pochi, Saa, Simu, Pipi, chocolate, mikufu, pete, shati, vitu vya urembo vya kuvaa vilivyonakishiwa kwa vito vya dhamani na dhahabu, begi, ua waridi ambalo halijanyauka, Mengine unajua mwenyewe au utaongozwa na mazingira na hali halisi.
Post A Comment: