Klabu ya Barcelona Jana usiku imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mfalme nchini Hispania (Copa del Rey) kwa kuicharaza klabu ya Valencia goli 2-0

Magoli ya Barcelona yamefungwa na Ivan Rakitic na mshambuliaji mpya wa Barcelona Philippe Coutinho ikiwa ni goli lake la kwanza tangu ajiunge klabuni hapo akitokea Liverpool.

Barcelona wamefanikiwa kufuzu kwa aggregate ya magoli 3-0 baada ya mchezo wa kwanza Barca kushinda goli 1-0.
Barcelona itakutana na Sevilla kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme itakayochezwa Aprili 21, 2018.

Hii inakuwa fainali ya 5 mfululizo kwa Barcelona ambapo imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Hispania kucheza fainali nyingi mfululizo na wamefanikiwa kuchukua kombe hilo mara nne.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: