MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema wakati wakiendelea kumchunguza Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel, Zachary Kakobe, mnamo Januari 24, 2018, Askofu huyo alimuandikia barua Rais Dkt. John Magufuli kumuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi na matamshi ya dharau kuwa ‘ana pesa nyingi kuliko Serikali’.

Hayo yamesemwa leo na Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere, wakati akizunumza na wanahabari jijini dar es Salaam akitoa ripoti ya uchunguzi huo.
Akihubiri wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi, Desemba 24, mwaka jana, askofu huyo alisema yeye ni tajiri zaidi ya serikali ya Tanzania na baadaye kusema kuwa utajiri anaomiliki kwa sasa ni zaidi ya serikali nyingi duniani jambo ambalo liliwafanya TRA wamchunguze.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: