Kikosi cha Yanga kitashuka Uwanja wa Azam Complex Chamazi Jumamosi usiku kuikabili Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu.
Mechi hiyo itakuwa ndiyo mara ya kwanza kwa kikosi cha Jangwani kucheza kwenye uwanja huo usiku tangu uanzishe.

Mechi zingine zitakazopigwa Jumamosi ni Stand na Ndanda, Mbeya City na Mtibwa Sugar pia Kagera Sugar na Lipuli.
Simba watakuwa na kibarua mbele ya Majimaji wakati Singida United watakutana na Prisons.

Mechi zingine zitachezwa keshokutwa Ijumaa, ambapo Ruvu Shooting watakutana na Mbao FC wakati Mwadui watavaana na Njombe Mji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: