Baadhi ya wazazi katika halmashauri ya mji wa wa Mbinga mkoani Ruvuma wameshindwa kulielewa agizo la Rais Dkt John Magufuli la kufuta michango katika shule za msingi na sekondari na kuvamia shule wakidai kurejeshewa michango yao.
Kufuatia hali hiyo Baraza la halmashauri ya mji wa Mbinga limeitisha kikao cha dharura kujadili changamoto hizo na namna ya kuzitatua huku Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mbinga Bw.Donald Msigwa akiwataka madiwani kutopingana na agizo la Rais katika majadiliano hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Mbinga Mheshimiwa Egno Kipwere amesema agizo la Rais halijahalalisha wananchi kudai kurejeshewa michango waliyochangia na halijafuta michango waliyokubaliana wenyewe kuchangia.
Post A Comment: