Wananchi wa miji ya Shinyanga na Kahama wamekosa maji kwa siku 7 baada ya TANESCO kukata umeme kwenye mtambo wa kusukuma maji uliopo Ziwa Victoria.
Hii ni kutokana na deni la zaidi ya Sh. bilioni 2 inalodiwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira miji ya Shinyanga na Kahama (KASHWASA) na TANESCO. Soma
Umeme huo umekatwa kutoka chanzo cha mradi mkubwa kinachoanzia Ziwa Victoria unaohudumia wilaya tano za Misungwi na Nangudu, Kahama ,Kishapu na Shinyanga
TANESCO walikata umeme kutoka mtambo wa kuyasukuma maji hadi kwenye tenki kuu lililopo mlima wa Mabale
Viongozi kutoka KASHWASA wamesema wanawasiliana na Wizara na wanaomba wananchi kuwa wavumilivu
Wakazi wa mji wa Shinyanga wamesema waamka saa kumi na mbili asubuhi kwa ajili ya kutafuta maji na wananunua dumu moja la maji kuanzia shilingi 500 hadi 1000 na maji yenyewe yanakuwa ni machafu
Chanzo: Azam Tv
Post A Comment: