Katika kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Siha Kata ya Ngarenairobi, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole, amewaeleza wananchi wa Jimbo la Siha kuwa kuichagua CCM ni kuchagua maendeleo ya watu wa Jimbo la Siha.
Kampeni za kumnadi mgombea Ubunge wa CCM, zimehudhuriwa na umati wa wananchi wa wilaya ya Siha na Viongozi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti Mkoa wa Kilimanjaro Ndg. Patrick Peter Boisafi.
Katibu Mwenezi wa CCM amewaeleza wananchi, CCM inazifahamu changamoto za Jimbo la Siha ikiwa ni pamoja na suala la Ardhi, Huduma za afya na Suala la Shule ya Msingi na Sekondari.
Hivyo CCM ipo tayari kuzitatua changamoto hizo kwa wakati baada ya timu ya kuleta maendeleo kukamilika endapo wananchi wa Jimbo la Siha watamchagua kwa kura nyingi Dr Godwin Mollel kuwa Mbunge wa Siha kwa tiketi ya CCM.
Baada ya Dr. Mollel kutazama na kuona maendeleo yanacheleweshwa na Chama chake cha awali (Chadema) ambacho hakina dira wala muelekeo, Dr Mollel ameamua kujumuika na timu ya ushindi, waheshimiwa wananchi mchagueni Dr Mollel awatumikie ,awahudumie na awaletee maendeleo. Lazima ifike wakati tunapomtafuta mwakilishi ambaye anakwenda kuwawakilisha wananchi, tupate mwakilishi ambaye akiwatazama usoni anajua shida na changamoto zenu. Amesema Ndg. Polepole.
Katika mkutano huo wananchi wameelezwa juu ya tabia za vyama vya upinzani kukosa msimamo katika kusimamia agenda za wananchi na kuwasihi kutovichagua vyama hivyo. *Chama kisicho kuwa na msimamo hakipaswi kupewa dhamana yoyote ya uongozi. Walisema hatuna shirika la ndege, walisema kuhusu baadhi ya watu ni mafisadi, walisema Rais asisafiri kwenda nje ya nchi, walisema kuhusu madini na sasa tunaye Ndg. Magufuli anayechukizwa na rushwa na kila aina ya ubadhirifu wa mali za umma, anatenda sawasawa na matakwa ya wananchi wa Tanzania lakini wapinzani sasa wanasema kinyume na kupinga kila jema. Amesisitiza Ndg. Polepole.
Huu ni muendelezo wa ziara za Katibu Mwenezi wa CCM zenye lengo la kujenga Chama pamoja na kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015- 2020.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
SIHA, KILIMANJARO
Post A Comment: