Aweso alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Shinyanga na wakazi wa Kijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga na kusikitishwa na mwenendo wa utekelezaji usioridhisha wa mradi wa maji kijijini hapo.
‘‘Nikuombe sana Mkurugenzi wa Halmashauri, hakikisha mnawapa kazi wakandarasi watakaohaikisha miradi inakamilika kulingana na mikataba yao, miradi mingi ya Serikali imekua haina manufaa kwa wananchi na kukosa tija kwa taifa kwa sababu tunawapa wakandarasi wazembe, wanaokosa uzalendo na kutokujali maslahi ya taifa.’’
‘‘Mfano mzuri ni mradi huu wa Mendo ulioanza kutekelezwa tangu Aprili 2014 na ulitakiwa kukamilika Disemba 2017, lakini bado haujakamilika wakati Serikali imeshaingia gharama ya zaidi ya Sh. mil 300. Jambo ambalo si sahihi, hivyo naagiza ifikapo mwisho wa mwezi huu uwe umeshakamilika na wananchi wapatao 2199 waanze kupata maji,’’ aliagiza Naibu Waziri Aweso.
Naibu Waziri Aweso ameanza ziara ya siku 5 mkoani Sinyanga inayolenga kukagua maendeleo ya miradi ya maji na kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa nia ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati na wananchi wa mkoa huo wanapata huduma ya maji ya uhakika kulingana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitembeleaKijiji cha Mendo, mkoani ShinyangaNaibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiongea na wananchi waKijiji cha Mendo, mkoani ShinyangaNaibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mtambo wa majiKijiji cha Mendo, mkoani Shinyanga
Share To:

msumbanews

Post A Comment: