Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMAJoseph Haule ambaye pia ni maarufu kwa jina la Prof Jay, polisi Mkoani Morogoroimethibitisha kuwatafuta yeye na baba yake mzee Steven Haule.
RPC Morogoro Urichi Matei amethibitisha kumtafuta Joseph Haule na baba yake mzee Steven Haule kwa madai ya kukutwa kwa matrekta ambayo ni mali ya SUMA JKT yakiwa nyumbani kwa mzee Steven Haule.
Matrekta hayo yanaripotiwa kuwa walinyang’anywa madereva na kudaiwa yanarudishwa SUMA JKT ambao ndio wamiliki kwani bado yandaiwa hayamaliziwa mkopo ila baadae yakakutwa nyumbani kwa mzee Steven Haule.
“Hizi trekta zimekutwa nyumbani kwa mzee Steven Haule ambaye ni baba yake na huyu mbunge Joseph Haule maarufu kama Prof Jay, zimefika pale kwa namna gani hatujui ila kwa sasa hivi nimemuelekeza OCD kumtafuta bwana Steven Haule na Joseph Haule ili watusaidie zile trekta kama ni mali yao au wamezipataje”>>>RPC Urichi Matei

Share To:

msumbanews

Post A Comment: