Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mhe HAMAD MASAUNI ahamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo kushiriki kufanikisha kupata vifaa vya ujenzi za nyumba za polisi mkoa wa pemba zanzibar ambapo wadau mbalimbali wamechangia milioni 400 zitakazo gharimu ujenzi wa nyumba za askari polisi.

 Mheshimiwa MASAUNI amesema upatikanaji wa makazi bora ya askari polisi utaongeza ufanisi mkubwa wa kazi kwa polisi   na kuweza kufanya majukumu yao kwa kujituma na kwa ufanisi mkubwa, Pia amesema askari wote wa nchi nzima wanachangamoto za makazi  na kama SERIKALI wana mpango mzuri wa kukabiliana na changamoto hizo za makazi na kuhakikisha askari polisi wanakuwa na makazi bora ya kuishi.

Mh: MASAUNI Alimkabidhi mkuu wa mkoa wa kusini pemba, MWAJUMA MAJID ABDALLA vifaa vilivyo changwa  na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya nyumba za polisi vifaa hivyo ni pamoja na
mifuko ya saruji
Ndoo za rangi
Mabati pamoja na nondo mhandisi MASAUNI alimkabidhi pia mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba  OMARI KHAMIS OTHMAN vifaa vya ujenzi

Amesema wadau wamechangia shilingi million 4oo kwa ajili ya nyumba za polisi katika mikoa iyo   na kuhasa usimamizi bora juu ya nyumba izo za polisi.

✍jumanne Abdul
     0757889297
Share To:

msumbanews

Post A Comment: