Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jengo jipya makao makuu ya Umoja
wa Afrika ambalo limepewa jina la rais mwanzilishi wa taifa la Tanzania,
Julius Nyerere.
Jengo hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.
Litakuwa
makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa
wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu
juhudi za kulinda amani za AU.
Ujenzi
wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na
linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.
Jengo
hilo lina ofisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na
Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na
vyumba vya shughuli za pembeni.
Mwalimu
Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa
viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni
Umoja wa Afrika (AU).
Bi Merkel amezuru nchi kadha za Afrika zikiwemo Mali na Niger. Hapa anaonekana na Rais Mahamadou Issoufou wa Niger.
Alishiriki
sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa
ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.
Mwalimu
Nyerere alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za
Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi
mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).
Post A Comment: