Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inaendelea leo Oktoba mosi 2016 kwa mchezo mmoja mkali wa kukata na shoka unaozikutanisha Timu mbili ambazo ni kongwe kwa soka hili la bongo
watani wa jadi, Young Africans na Simba katika dimba la Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo, umekuwa na hamasa ya aina yake.
Lakini kesho  siku ya Jumapili, michezo itakuwa mitano ambako Mbeya
ya City itaikaribisha Mwadui kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.
Mbao baada ya kucheza na Ruvu Shooting wiki iliyopita, ilibakia Mlandizi mkoani Pwani kusubiri kucheza na JKT Ruvu Jumapili kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi wakati Kagera itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera

Share To:

msumbanews

Post A Comment: