Wakazi wakiangalia mwili wa mtu aliyeuawa katika wilaya ya Nyakabiga, Bujumbura, Desemba 12, 2015
Serikali
ya Burundi imechukua uamuzi wa kusitisha ushirikiano wake na Ofisi ya
Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, inayotuhumiwa kula njama katika
kuandaa ripoti ya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa (EINUB).
"Kufuatia
njama ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu nchini Burundi,
katika maandalizi ya ripoti ya uongo na yenye utata ya Wataalam
wanaodaiwa kufanya Uchunguzi Huru wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi
(EINUB), Serikali ya Burundi imeamua kusitisha ushirikiano wowote na
kushirikiana katika miundo yake yote, pamoja na Ofisi ya Umoja wa
Mataifa ya Haki za Binanadamu hadi itakapotangazwa tena.
"Maneno
haya yameonekana kwenye tangazo lililosainiwa Jumanne hii Oktoba 11,
2016 na Philippe Nzobonariba, katibu Dola na Msemaji wa serikali.
Kwa
mujibu wa tangazo hili, uamuzi huo ulifahamishwa maofisa wa Ofisi hii
wakati wa kikao cha kazi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa wa Burundi Alain Aimé Nyamitwe, Jumatatu hii, Oktoba 10,
2016."Kwa maana hii, Burundi inaomba kwa kusubiri, Ofisi ya Umoja wa
Mataifa ya Haki za Binadamu kuteua timu itakayoendesha mazungumzo kuhusu
makubaliano ya makao makuu, ambayo yataweka wazi majukumu yake, muda na
idadi ya wafanyakazi wake nchini Burundi," imeongeza taarifa
hiyo.Uamuzi huu unakuja baada ya maandamano mjini Bujumbura mwishoni mwa
wiki iliyopita mbele ya makao makuu ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya
Haki za Binadamu ambapo waandamanaji waliomba ofisi hiyo kufungwa haraka
iwezekanavyo.
Ripoti
ya EINUB ilikuwa chanzo cha azimio HRC33 lililochukuliwa na Baraza la
Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo linaomba kuundwa kwa Tume ya
Kimataifa ya Uchunguzi wa ukiukaji wa haki zabinadammu nchini Burundi.
Azimio ambalo lilikataliwa na serikali ya Burundi, ambayo inautuhumu
Umoja wa Ulaya kuwa imeandaa na kupanga njama dhidi yake.
Post A Comment: