Home
BURUDANI
Amber Lulu adai yeye na Young Dee walikuwa kwenye mahusiano
 
             
    
Ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali. Ukweli wafahamika 
baada ya mara kadhaa rapper Young Dee kukanusha kuwahi kuwa na mahusiano
 na video vixen kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu.
Akiongea na U-Heard ya Clouds FM, Amber Lulu amefunguka ukweli kwa 
kusema kuwa amekuwa na mahusiano na rapper huyo kwa tangu miaka minne 
iliyopita wakati akiwa mkoani Mbeya.
“Marafiki zangu wanajua ni jinsi gani nilivyokuwa naishi naye, 
mara ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio nilienda kumtoa ndugu zake
 wote walikataa kwenda, Mimi nimeenda. Matatizo yangu yeye anayafurahia 
ina maana. Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi wangu ni mtu
 ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,” amesema Amber.
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 Back To Top
 
Post A Comment: