Mkutano wa Igad ulifanyika chini ya ulinzi mkali
Mkutano wa Igad ulifanyika chini ya ulinzi mkali
Viongozi wa nchi wanachama wa muungano wa maendeleo Afrika Mashariki na pembe ya Afrika (IGAD) wamefanya mkutano wa kihistoria mjini Mogadishu, Somalia.
Imekuwa mara ya kwanza kwa mkutano kama huo kufanyika mjini Mogadishu tangu kuanzishwa kwa muungano huo miaka 30 iliyopita.
Viongozi kutoka Kenya, Uganda , Ethiopia na Somalia walihudhuria mkutano huo.
Bango la kukaribisha washiriki wa mkutano huo
Bango la kukaribisha washiriki wa mkutano huo
Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hao walitoa hakikisho kuwa jamii ya kimataifa na washirika wako tayari kuisadia Somalia, kuhakikisha kuwa uchaguzi umefanyika wakati ufaao kuambatana na matakwa wa watu wa Somalia.
Pia suala la kurejeshwa kwa wakimbizi wa Somalia kutoka nchini Kenya ambalo limekuwa likiendelea kwa miaka mitatu sasa. Viongozi hao sasa wametoa wito wa kutaka kufanyika zoezi hilo kwa njia ya amani.
Bendera za mataifa wanachama wa Igad
Bendera za mataifa wanachama wa Igad
Adha serikali ya Somalia ilitangaza kuwa imeondoa marufuku ya usafirishaji wa miara kutoka nchini Kenya. Marufuku hiyo ilitangazwa wiki moja iliyopita na imesababisa hasara ya mamilioni ya dola kwa wakulima wa miraa nchini Kenya.
Wengi wa wanachama, Ethiopia, Uganda na Kenya, wamechangia wanajeshi katika kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika ambacho kinasaidia serikali kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabab. BBC
Share To:

msumbanews

Post A Comment: