ARUSHA MEYA MSTAAFU WAFIKISHWA KORTINI

Naibu Meya mstaafu  na pia aliyekuwa Diwani wa kata ya Daraja mbili Prospa Msofe na Afisa mtendaji wake Modesta Lupogo wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma tofauti tofauti zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma

Kesi hiyo ni kesi no 379 iliyoongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Ruwenkiza na wakili wa TAKUKURU Monika Kijazi akishirikiana na Rehema Mteta ambapo wamesema

Vigogo hao wanakabiliwa na kesi tatu ambapo kesi ya kwanza ni ya  Afisa mtendaji Modesta Lupogo aliwasilisha nyaraka za uongo za mapato na matumizi kuanzia October hadi December 2013 ya shilingi million 8 kuwa zilitumika kwenye  mradi wa maji katika mtaa wa Alinyanya na Sanare kata ya  Daraja mbili na huku fedha hizo hazikutumika katika mradi huo bali zilitumika kwa maslahi ya mtu binafsi

Kesi ya pili inawahusu watuhumiwa  wote wawili ambapo walishiriki kutenda kosa la Ubadhilifu wa fedha za umma ambapo katika sheria ya TAKUKURU ni kosa  kifungu 32

Kesi ya tatu inamuhusu Naibu Meya mstaafu na aliyekuwa diwani wa kata ya Daraja mbili Prospa Msofe kwa kuhusika na Ubadhilifu wa fedha za umma kuanzia October mosi hadi November 30 ambapo ni kosa katika sheria ya TAKUKURU  kifungu 28(1)kuwa million 8  hazikutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa na halmashauri

Washtakiwa wote wamekidhi masharti ya dhamana ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini wawili wawili watakaosaini bondi ya shilingi million mbili ,kitambulisho cha kazi kinachotambulika na uchunguzi umeshakamilika hivyo  hoja za awali zitasomwa October 11 


 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: