SONGEA WAFANIKIWA KUDHIBITI KICHAA CHA MBWA.

 KATIKA kuhakikisha kuwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa unadhibitiwa katika Manispaa ya Songea,Idara ya Mifugo na Uvuvi katika Manispaa hiyo imeanza kampeni za kuwasaka mbwa wote wanaotembea mitaani hovyo ambapo kuanzia Januari hadi Juni 2016 wamefanikiwa kuua mbwa 169.Katika kipindi hicho watu takriban 20 wameumwa na mbwa kati yao ni mtu mmoja tu amepoteza maisha baada ya kuathirika na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.Kata 13 kati ya 21 za Manispaa hiyo ndiyo zinakabiliwa na mbwa wanaotembea hovyo mitaani.Moja ya mikakati inayochukuliwa ni kutumia sheria ndogo kuwatoza faini  kati ya sh.50,000 hadi 100,000 wale wote ambao wanawaacha mbwa wao hovyo mitaani bila kuwafunga.


www.msumbanews.blogspot.com
Share To:

msumbanews

Post A Comment: