MTANGAZAJI MPYA CLOUDSFM.

Maisha
ni safari na hatutakiwi kukata tamaa kwa kuwa hatujui kesho yetu.
Ukiisikia historia ya maisha ya mchekeshaji ambaye kwa sasa amegeuka
kuwa mtangazaji wa Clouds FM, Kicheko unaweza kutokwa na machozi kama
huna uvumilivu.
Awali
Kicheko alikuwa member wa Ze Comedy ya EATV baada ya kuchaguliwa kwenye
shindano la kutafuta wasanii watakaogiza kwenye kipindi hicho ambapo
alidumu hapo kwa muda wa miaka isiyopungua miwili.
Waswahili
wanasema “acha kazi, uone kazi, kupata kazi, ilivyokuwa kazi,” lakini
kwa Kicheko haikuwa ngumu kwake kuacha kazi EATV ya uchekeshaji baada ya
kuchukua maamuzi ya kuandika barua ya kuacha kazi kwenye uongozi wa
kampuni hiyo April, 2014 huku akiwa hana kazi. Lakini pia mtangazaji
huyo amepinga taarifa za kuwa alifukuzwa kazi kwenye kituo hicho cha
runinga.
Baada
ya muda kupita Kicheko alifanikiwa kupata shavu la utangazaji kwenye
redio ya EFM akiendesha kipindi cha Singeli ‘Genge’ ambacho kimekuwa
kikipendwa zaidi na mashabiki mitaani na kufanya brand yake kuanza kuwa
kubwa.
Kumbe
ilikuwa ni dhahabu huku wengi wakidhani lilikuwa ni jiwe, rangi yake
ilifichwa na vumbi ndiyo maana kila mpita njia alilidharau kabla ya EFM
na hatimaye Clouds FM kuliokota jiwe hilo na kulisafisha na hatimaye
sasa rangi yake halisi imeonekana na kila mtu ameanza kulitamani tena.
Akikaribishwa
kwa mara ya kwanza leo kwenye ofisi za Clouds Media (mjengoni) kwenye
kipindi cha ‘Leo Tena’ mtangazaji huyo ameelezea historia yake kidogo
huku akidai kuwa aliwahi kuwa mwizi huko nyuma. “Mwanzo nilikuwa mwizi,
mkabaji. Unajua haya ni maisha tu,” amesema Kicheko.
Kwa
sasa Kicheko amepewa heshima kubwa na watu wa mtaani ikiwa ni pamoja na
kumpa jina la ‘Rais wa Uswazi’ kutokana na support yake anayoitoa
kwenye muziki wa Singeli ambao umeonekana kukubalika zaidi kwa sasa huku
akiwa na wanachama 489 kwenye kikundi chake.
Mchekeshaji huyo anatarajiwa kuanza kazi kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uswazi Flava’ hapo Clouds FM.
Back To Top
Post A Comment: