Mwanamuziki Beka Ibrozama amefunguka sababu kubwa ya kuamua kuimba wimbo wake mpya wa ‘Mwanza’ kwa kutumia lugha ya Kisukuma


Akizungumza na eNEWZ, Beka amesema kuwa muziki ni melodi na wala sio maana na ndio maana hata tunasikiliza nyimbo za wanamuziki wa bolingo kutoka Congo ambapo hatujui maana yake lakini tunaupenda na kucheza.
“Muziki mzuri ni melodi, Tafsiri utakuja kujua baadaye. Kwakuwa tunaishi na Wasukuma basi utakutana na hata mmoja atakupa maana. Kwahiyo mimi ninaamini muziki mzuri ni melodi na tafsiri itafuata.” Alisema Beka.
Pia Beka amefafanua kuwa wimbo wake huo unahusu historia ya watu ili mtu asisahau alipotoka kwakuwa tu anaishi mjini.
Pia Beka mbali na kusikika kwenye muziki, amesema wadau ambao wanapenda muziki wake ndio walikuwa wakimuunga mkono kwa mchango wa kifedha katika band yake ambayo inathamani ya milioni themanini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: