Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob leo amekabidhi ramsi ofisi baada ya juzi madiwani wa baraza hilo kugawanywa kwenda katika Manispaa ya mpya ya Ubungo na wengine kubaki Kinondoni.

Hatua hiyo, Manispaa ya Kinondoni inafuatia uamuzi wa Serikali kuzigawa Kinondoni  na Temeke ambazo zimezaa wilaya za Ubungo na Kigamboni.

 

Baada ya kukabidhi ofisi hiyo Jacob aliwashukuru watumishi, madiwani na waandishi wa habari kwa ushirikiano walioinyesha katika kipindi cha miezi saba akiwa kiongozi.

“Narudi Ubungo home sweet home (nyumbani ni nyumbani), nasubiri ridhaa ya chama nikipitishwa,  nitagombea tena nafasi hii,”anasema Jacob.

 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: