Maswali yameibuka nchini Afrika Kusini kuhusu mkopo aliopewa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, na benki isiyo maarufu ya VBS kulipa deni lililotokana na ukarabati uliofanyiwa nyumba yake binafsi huko Nkandla.

Ofisi ya rais ilitoa taarifa siku ya Jumatatu, ikitangaza kuwa bwana Zuma alikuwa ametuma fedha hizo ambazo ni zaid ya dola 500,000 kweneda benki ya SARB. Hii ni kufuatia amri iliyotolewa na mahakama ya katiba mwishoni mwa mwezi Machi.

Bwana Zuma atalipa mkopo huo ndani ya kipindi cha miaka 20 inayokuja.

 

Kulingana na magazeti ya nchi hiyo, baadhi yanauliza ni vipi Zuma mwenye umri wa miaka 74 aliweza kupata mkopo huo ulio zaidi ya mapato yake na ikiwa ni kisa cha kutoa mkopo kwa njia ya kiholela.

Benki hiyo inayomilikiwa na watu weusi inaripotiwa kuwa na matawi manne tu kote nchini humo.

Wakati uo huo chama cha upinznania cha Democratic Alliance kimetaka kuona ahakaiksha kuwa deni hilo limelipwa.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: