MKUU WA MKOA WA ARUSHA  MRISHO GAMBO

Leo tumesikiliza kero za wamiliki na waendesha Noah Mkoani Arusha. Walikuwa wamezuiliwa kupata leseni pamoja na kuruhusiwa kusafiri umbali usiozidi Km 50 tu. Tumekutana wadau wote na kukubaliana waendelee kupewa Leseni kuanzia leo na safari zao zibaki kama kawaida. Wamekubali kupunguza idadi ya abiria kuwa nane na Polisi wamewapongeza watu wa Noah kwa kufuata sheria za barabarani na kukiri kuwa rekodi inaonyesha tatizo la ajali kwa watu wa Noah ni dogo sana. Nawatakia heri katika juhudi zao za kuendelea kujitafutia riziki kihalali.www.msumbanews.blogspot.com

 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: