Na John Walter-Manyara

Jamii imetakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa ya maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Maarufu Mkwaya wakati akifungua maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Mkoa wa Manyara yaliyoandaliwa na klabu ya Waandishi wa Habari mkoani hapa Mei 9,2022.

Mkwaya amesema kupitia mitandao ya kijamii mtu anaweza kufanya Biashara ya kuuza au kununua,kutangaza vivutio mbalimbali kwa faida ya Taifa kuliko kuchapisha Mambo yasiyo na maadili mema kwenye jamii.

Amesema wapo baadhi ya watu wasio waaminifu wasiozingatia  matumizi sahihi ya mitandao hiyo na kusababisha upotoshaji kwa wanaotumia  mitandao hiyo kwa ajili ya kujifunza na kuhabarika.

Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari hufanyika kila Mei 3 ya kila mwaka ambapo kitaifa yalifanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa mada zinazojadiliwa  katika maadhimisho hayo, ni pamoja na uandishi wa habari na changamoto za kidijitali, matumizi ya teknolojia na usalama mtandaoni.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni uandishi wa habari na changamoto za kidijitali.

Katibu wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Manyara Jaliwasson Jasson akizungumza jambo katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, yaliyoadhimishwa mjini Babati Mei 9 mwaka huu.

Share To:

Post A Comment: