Mradi mkubwa wa ujenzi wa mabwawa ya ufugaji samaki TANLAPIA Ltd, uliopo Nianjema ,Bagamoyo, Mkoani Pwani ukikamilika unalenga kusaidia wafugaji wa samaki aina ya Sato nchini na Ukanda wa Sahara , kwani utatumia teknolojia ya kisasa kuongeza uzalishaji na kupunguza athari za Mazingira.


Mradi huo wa kimkakati unatarajia kugharimu dollar milioni 19 sawa na sh.Bilioni 44.6 fedha ya kitanzania Hadi kukamilika kwake.

Akisoma taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahir Geraruma, wakati alipoweka jiwe la msingi kwenye mradi huo ,Meneja wa Mradi ,Farida Bozohera alisema ,Hadi kufikia mwezi April mwaka huu mradi umeshatumia sh.bilioni 11.5 .

"Mradi huu ukikamilika tutatumia teknolojia ya kisasa inayolenga kuongeza uzalishaji na kupunguza athari za Mazingira, kwa wafugaji wa samaki aina ya sato katika nchi zilizo Kusini mwa Ukanda wa Sahara.:;"alisema Farida.

Awali akipokea Mwenge huo ukitokea Halmashauri ya Chalinze, kwenye viwanja vya shule ya msingi Fukayose, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selenda alisema, Jumla ya miradi 11 yenye thamani ya sh.Bilioni 46.308.2 katika kata nne imetembelewa.

Nae Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah alieleza ,miradi 25 yenye thamani ya Bilioni 47.2 imepitiwa na mwenge huo katika Halmashauri mbili za wilaya hiyo.

Alieleza ,wilaya hiyo ina Halmashauri hizo mbili ambapo Halmashauri ya Chalinze imetembelewa miradi 14 iliyogharimu milioni 937.8 na Bagamoyo miradi 11 yenye thamani ya Bilioni 46.3.

Akielezea kuhusu mradi huo wa ufugaji samaki Zainab alibainisha ,Ni uwekezaji mkubwa katika Halmashauri ya Bagamoyo, Afrika Mashariki na kati na Ukanda wa Sahara.

Miradi mingine iliyopitiwa ni pamoja na mradi wa upanuzi wa maji kijiji cha Fukayose, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la upasuaji na wodi ya wazazi na barabara kiwango cha Pavement blocks mita 880.

Mwenge wa Uhuru uliingia Mkoani Pwani,"; Mei mosi na kutembelea miradi 111 yenye thamani ya sh.Bilioni 69.2 ,kwenye Halmashauri Tisa ambapo Mei 10 mkoa huu utaukabidhi Mwenge huo Jijini la Dar es Salaam.

Share To:

Post A Comment: