Tigo Tanzania yashirikiana na Shirika la Reli Tanzania - TRC kudhamini zoezi la ujenzi wa kipande cha reli ya kisasa yani Standard Gauge Railway (SGR) kipande cha Tabora-makutupora. Ikiwa lengo ni kuendeleza uhusiano mwema na serikali katika kuendeleza sekta ya miundombinu. Zoezi la uzinduzi limefanyika leo tarehe 12 April 2022 katika mkoa wa Tabora. 

Tigo inaendelea na itaendelea kutoa huduma kidigitali ya tiketi mtandao kwa watumiaji wa reli ambapo wanaweza kufanya booking za tiketi zao kupitia tovuti ya https://booking.trc.co.tz/ na kufanya malipo ya tiketi hizo kirahisi na haraka kupitia Tigo Pesa.

Tunajivunia uwepo wa huduma za Tigo Pesa kwa Makampuni mbalimbali yaani Corporate Solution ambapo hurahisisha malipo kirahisi, kwa usalama na kwa mkupuo kwenda kwa watu wengi zaidi mitandao yote Tanzania nzima. Kupitia huduma hii, TRC pamoja na washirika wake kama kampuni za ujenzi kama vile Yapi Merkezi utawezesha malipo ya vibarua na malipo mengine tofauti kirahisi, kidigitali na kwa usalama zaidi na kwa mkupuo kupitia huduma ya Tigo Pesa Corporate Solution.

Uhusiano Baina ya Tigo na TRC utasaidia kuendelea kwa huduma za kidigitali hasa malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kupitia Tigo Pesa ‘Lipa Kwa Simu’ kwa watumiaji wa mitandao yote kwa urahisi na usalama zaidi.


Share To:

Adery Masta

Post A Comment: