Muungano wa AXIAN Telecom na Rostam Aziz leo umetangaza kukamilika kwa mchakato wa umiliki wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania Public Limited Company (Tigo na Zantel) katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mchakato huu unaleta takribani wateja milioni 14 wa simu za mkononi  kwa AXIAN Telecom na kuharakisha ukuaji wa kampuni hii barani Afrika ambapo kwa sasa imefika nchi nane katika bara hili.

 Mpango kabambe wa ukuaji na wenye matumaini wa muungano wa AXIAN Telecom unajumuisha uwekezaji mkubwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ili kuimarisha ubora wa huduma zitolewazo na kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC.

*    Kwa kununuliwa kwa MIC Tanzania PLC, AXIAN Telecom inafungua ukurasa mpya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunayo furaha kuanza safari hii ya kusisimua na wenzetu wa hapa (Tanzania) na ninaamini kwa pamoja tutafanikisha mambo makubwa yatakayoendelea kuongoza mapinduzi ya  kidijitali hapa nchini. Tunatoa shukrani zetu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutusaidia kufanikisha mchakato huu, tunatarajia kuendelea kushirikiana kwa pamoja.

Hassanein Hirdjee,  Mwenyekiti wa AXIAN Telecom.

Muungano wa AXIAN Telecom umeweka vipaumbele vinne  (4) muhimu katika kutekeleza majukumu yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:

 

·         Kuendeleza mabadiliko ya kidijitali nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa na kutoa huduma zinazowanufaisha mtumiaji mmoja mmoja na makampuni ya Kitanzania. Muungano huu una uwezo wa kutumia teknolojia za mtandao wa kasi na nyaya za chini ya ardhi ambazo zitaleta  mawasiliano ya haraka kati ya Watanzania na kwingineko duniani.

 

·         Kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za mawasiliano na kuongoza ujumuishwaji wa kidijitali kwa kuwekeza kikamilifu kwenye ujenzi wa miondombinu ya mawasiliano.  Muungano huu unapanga kuimarisha upatikanaji na ubora wa mtandao  hasa kupitia teknolojia ya 4G.  

 

·         Kuongeza kasi ya ujumuishwaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi, kwa kuzingatia mafanikio ya huduma hizi kutoka kwenye kampuni zilizounganishwa ili kuendeleza zaidi huduma za kifedha kwa njia ya simu zinazolenga mahitaji ya wateja wa Tanzania. Umoja huo pia utahakikisha muungano huu unafaidika kupitia utaalamu wake wa kutoa huduma za kifedha za kiwango cha juu katika nchi zingine.

 

 

·         Kukuza na kuendeleza vipaji. Muungano huo unakusudia kukuza maendeleo ya taaluma za wafanyakazi na kuweka mkazo mkubwa kwenye mafunzo, kubadilishana uzoefu na kushirikishana maarifa ya pamoja miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC.

 

Muungano huu unajumuisha AXIAN Telecom na Bw. Rostam Azizi, mtanzania mfanyabiashara na mjasiriamali ambaye ana taaluma ya muda mrefu kwenye sekta ya mawasiliano  na amekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya sekta hii hapa nchini Tanzania. Bw. Azizi, akiwa kama Mwenyekiti ajaye wa MIC Tanzania PLC, atatoa mwongozo wa kimkakati na usimamizi wa kampuni na mfumo mzima wa uendeshaji na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wadau  wa sekta ya mawasiliano nchini Tanzania.

 

*     Tulipoanza safari yetu ya mawasiliano zaidi ya miaka ishirini iliyopita, suala kubwa lilikuwa kuunganisha watanzania kwenye huduma hii. Tulikuwa waanzilishi katika kujenga  mtandao wa huduma za simu, hasa katika maeneo ya vijijini, ambapo kwa sasa  Watanzania wenzangu wengi wanafurahia huduma hii. Tukitazama malengo ya pamoja na AXIAN Telecom, ni Dhahiri kuwa tutafanikiwa kuondoa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa huduma za kidigitali nchini kote,  tukizingatia mahitaji muhimu  kwa Watanzania na makampuni.

Rostam Azizi, Mwenyekitii MIC Tanzania PLC.

 Katika Toleo la dhamana la AXIAN Telecom lilifanikiwa na kukamilika Februari 2022, linaashiria matumizi ya mara ya kwanza ya mfumo wa escrow kwa kampuni binafsi inayofanya kazi barani Afrika na kuakisi sifa ya Tanzania kama  chaguo la wawekezaji. Mafanikio ya dhamana yanatoa ishara tosha kwa masoko yote kuwa wawekezaji wa kimataifa wana fursa za uwekezaji hapa nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla . AXIAN Telecom inafungua njia mpya kwa sekta binafsi barani Afrika kuhamasisha uwekezaji ili kuboresha maisha ya kila siku ya watu inayowahudumia.

 

Ikitumia utaalamu wake hasa katika kusambaza teknolojia za hali ya juu kama vile mitandao ya 5G na kuanzisha huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi zilizofanikiwa, AXIAN Telecom ina dhamira ya kuupa nguvu mfumo wa mawasiliano hapa Tanzania hasa katika kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma bora zaidi.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: