Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeendelea kuboresha Karakana zake 17 ambazo zipo katika mikoa mbalimbali nchini. Mpaka sasa karakana ya mkoa wa Dodoma tayari imefanyiwa maboresho makubwa ambayo yalifanyika 2019 na uzalishaji wa thamani unaendelea kwa upande wa milango na madirisha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Serikali inayoendelea mkoani Dodoma.

Baadhi ya miradi iliyonufaika na Karakana hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi katika eneo la Kisasa.

Faida zinazopatikana kutokana na uwepo wa Karakana hizi ni pamoja na kuzalisha ajira nyingi kwa Vijana wa Kitanzania, kupunguza gharama za ujenzi na ukamilishwaji wa kazi kwa wakati kulingana na mahitaji husika.

Katika shughuli za uzalishaji, Meneja wa Karakana na Ukarabati (TBA), Mbunifu majengo (Arch) Theresia Simon, ametaja baadhi ya changamoto wanazokutana nazo hasa katika karakana ya mkoa wa Dodoma ni pamoja na makadilio yasio na uhalisia yanayofanywa na baadhi ya wataalamu, “over specification” na kuchelewa kulipwa kwa wakati kazi zilizokamilika. Pamoja na hali hiyo, kazi kubwa imefanyika na baadhi ya changamoto zimeendelea kutatuliwa.

Karakana ya Dodoma imeendelea kutekeleza miradi mabalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Tume ya maadili ya watumishi wa umma, mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi ya viongozi zilizopo katika eneo la Kisasa pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba 150 za makazi ya watumishi wa Serikali unaoendelea katika eneo la Nzunguni
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: