Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utwala na bwalo la chakula katika shule ya sekondari kituntu ili mwakani 2023  ianze kupokea wanafunzi wa  kidato cha tano na sita.



Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Machi 28, 2022 wakati akiongea na Wanafunzi, Walimu na uongizi wa shule katika ziara ya kukagua maendeleo ya uanzishwaji wa kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Kitutu iliyopo Halmashauri ya wilaya Karagwe Mkoani Kagera.



Waziri Bashungwa amesema mchakato wa usajili na uanzishwaji na  kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari kituntu ulianza tangu mwaka 2015 ikilenga kuanzisha tahasusi za HGL na CBG.


Aidha, Waziri Bashungwa ameahidi kumaliza changamoto ya upungufu wa walimu wa sayansi, hisabati na sanaa katika shule hiyo wakati Rais atakapo Toa Kibali  cha ajira za Walimu 7,000 zinazosubiliwa itakayoenda sambamba na kufanyia kazi changamoto ya nyumba za walimu.



Pia, Amemuelekeza Mkurungenzi wa Halmashauri ya Wilaya karagwe kushughulikia changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo  kwa kutoa kipaumbele kupitia fedha za ndani ya Halmashauri ya Wilaya Karagwe.



Awali, Mkuu wa Shule ya Sekondari kituntu, Mwalimu Muganyizi Katatumba amesema kuwa kiu ya wananchi wa kata ya kituntu na wilaya kwa ujumla ni shule yao kuwa na kidato cha tano na sita maana wamejitoa kuchangia michango yao kwa ajiri ya kuongeza vyumba vya madarasa.

Share To:

Post A Comment: