Na Mustafa Leu.

COSTECH Tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia,muhimili na nguzo kuu ya  taasisi za utafiti wa maswala yote ya Sayansi nchini imejizatiti kuhakikisha wananchi wananufaika na uguduzi na utafiti unaofanywa na wanasayansi nchini na Kuharakisha mabadiliko yaharaka ya maendeleo  kwajamii ..

Kwa kipindi kirefu Utafiti na ugunduzi wa maswala mbalimbali ya kisayansi umekuwa ukifanyika maeneo mbalimbali nchini lakini umekuwa ni siri kubwa ambayo imeshindwa kuwafikia walengwa na hivyo kushindwa Kuleta mabadiliko yaliyokuwa yakitarajiwa kwa wakati.

Zipo changamoyo ,mbalimbali ambazo  zimesababisha matokeo ya tafiti hizo kutokuwafikia walengwa,ikiwemo lugha ngumu ya kitaalamu iliyotumika kuandika taarifa nayotumika na matokeo yake taarifa hizo kubakia siri ya watafiti

Kaimu mkurugenzi mkuu wa COSTECH, Daktari,Philibelrti Luhuga,anasema kutokana na changamoto hiyo ya matokeo ya utafiti kutokuwafikia walengwa na hivyo kuleta mabadiliko taasisi hiyo imekuja na suluhisho la kudumu

COSTECH,Imeamua kushirikisha na. kutumia vyombo vya habari ili viweze kuandika taarifa za matokeo hayo kwa lugha rahisi inayoeleweka kwa walengwa na hivyo matokeo ya tafiti na gunduzi yataleta mabadiliko ya haraka



Vyombo vya habari vikiwemo,radio,luninga majarida,magazeti,vipeperushi,mitandao yote ya kijamii itakuwa na. jukumu kubwa la kuandaa vipindi na. makala mbalimbali za kuelimisha umma kuhusu matokeo hayo ya utafiti na ugunduzi kutoka kwa wanasayansi waliopo kwenye taasisi mbalimbali nchini.

Tunawapongeza COSTECH kwa uamuzi wao wa kuvishirikisha vyombo vya habari hayo ni mafanikio makubwa Katika  utafiti ugunduzi na. ubunifu yatawezesha kupatikana matokeo ya haraka amboyo taifa linayangojea

Tayari wanahabari mikoa mbalimbali wameshaanza kunolewa na wengine wanaendelea kunolewa ili wawe na uelewa mkubwa wa maswala yatafiti na ugunduzi hayomar waandike kwa lugha nyepesi ambayo inaeleweka.



Watafiti hawapaswi kulaumiwa kwa kushindwa kutoa matokeo ya tafiti huo  ni mfumo  uliokuewepo tangia kale kwa kuwa umejengwa Kama mtafiti akisha kamilisha utafiti wake anauwasilisha kwenye mamlaka husika na yeye  hana nafasi au jukumu  la kuelezea popote.

Ni ukwell usiopingika kuwa kwenye
gunduzi watafiti na wagunduzi wanapotoa taatifa za mbalimbali zinazoelezea matokeo lakini mfumo uliokuwepo wa kutokuwapa nafasi ya kueleza matokeo umewanyima wananchi haki ya kufahamu na kushiriki kuleta madiliko kutokana na matokeo hayo.



Mfumo huo uliojenga usiri kwenye shughuli zote za kitafiti na gunduzi limekuwa ni tatizo la muda mrefu na wakati mwingine wananchi kushindwa kutambua na kuelewa watafiti wanafanya kazi gani na. hivyo ukaribu kati ya watafiti na wananchi unakosekana

Mkazo uliopo ni kuhakikisha kila taasisi inayojihusisha na utafiti wa kisayansi inatoa matokeo ya tafiti na gunduzi hizo iliyoandikwa kwa lugha rahisi na kuitangaza kupitia vyombo vya habari

Mara baada ya mafunzo hayo sasa kazi imebakia kwa wanahabari kufanya kazi,kuandika makala,na,kuandaa vipindi mbalimbali vinavyelezea matokeo ya tafiti ili kurahisisha na kuleta mabadiliko kwa jamii.


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: