Sunday, 19 December 2021

Waziri Ummy akagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Uyui.

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amekagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora.


Akiwa ziarani Wilayani humo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Jengo hilo la Utawala na kusema litakapokamilika litaboresha utoaji wa huduma katika Halmashauri hiyo.


Jengo la Utawala la Halmashauri ya Uyui mpaka kukamila kwake litagharimu takriban sh Bil 3 na mpaka sasa limefikia hatua ya umaliziaji.


Katika kukamilisha jengo hilo Kazi zilizopangwa kufanyika  ni ujenzi wa uzio, mgahawa, kihifadhio cha maji, maduka na kufanya landscaping.


Jengo hili linategemewa kukamilika Februari,2022.

No comments:

Post a Comment