Na. John Mapepele

Mkoa wa Mjini Magharibi umeibuka bingwa wa jumla wa mashindano ya Taifa CUP 2021 yaliyomakizika Jana Disemba 16, 2021 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yalifungwa na Waziri wa Habari,Utamaduni vijana na Michezo kutoka Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita ambapo alipongeza Kamati kwa uratibu mzuri wa mashindano haya yaliyoshirikisha pande zote za Muungano.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu mashindano ya mwaka huu ya Taifa CUP 2021 Yusuph Omary Singo Mkoa wa Arusha umekuwa wa mshindi pili wa jumla ukifuatiwa na Dar es Salaam.

Singo amesema mashindano haya yalishirikisha mchezo wa Soka kwa wanawake na wanaume, Netiboli, Riadha na Maonesho ya Sanaa za Muziki wa kizazi kipya na Singeli huku ikipambwa na vikundi vya Michezo ya jadi.

Kwa upande wa soka la wavulana Mkoa wa Mjini Magharibi ndiyo bingwa ukifuatiwa na Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa mkoa wa Ruvuma.Katika mchezo wa Soka kwa wanawake mkoa wa Arusha umeongoza ukifuatiwa na Dar na Mara.

Mchezo wa Netiboli mkoa wa Mjini Magharibi ni wa kwanza ukifuatiwa na Dar na Dodoma wakati kwenye mchezo wa Riadha Kusini Unguja ndiyo bingwa ukifuatiwa na Arusha na Kilimanjaro.

Kwa upande wa maonesho ya Sanaa za Muziki wa kizazi kipya Pwani umeongoza ukifuatiwa na Mbeya na Dar wakati kwenye Muziki wa Singeli Mkoa wa Morogoro umeongoza, wa pili ni Dar na Mjini Magharibi.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: