Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI



Wanafunzi 3,404 waliofauli darasa la saba katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wanategemea kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja kutokana na ujenzi wa madarasa  47 yanayojenhwa katika Halmashauri hiyo.


Akiwa ziarani Wilayani humo  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amekagua ujenzi wa vyumba 7  vya madarasa katika shule ya Sekondari  Gumangwa kwa niaba ya vyumba vyote 47 vilivyojengwa katika Halmashauari hiyo.


Kutoka katika mradi wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambamo dhidi ya UVIKO-19 Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imepoeka shilingi Milioni 940 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 47 katika shule za Sekondari Wilayani humo.


Akiwa shuleni hapo Waziri Ummy ameridhishwa  na ujenzi wa madarasa hayo  na amepongeza Uongozi wa Manispaa ya Singida kwa usimamizi makini wa ujenzi wa madarasa hayo.


Naye Makamu Mkuu wa  shule ya  Sekondari ya Gumangwa Mwl. Lucas Egugu amesema wanafunzi waliomaliza kidato cha nne katika shule hiyo ni  77 na waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza ni 245 lakini kwa ujenzi wa madarasa hayo 7 yatapawezesha wanafunzi wote kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja.


Pia amemshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha walizopata kwa kuwa zimeongeza fursa za Elimu kwa watoto wote wa Kitanzania kupata elimu yao kwa wakati.

Share To:

Post A Comment: