Mwandishi Wetu.

Ikiwa ni wiki kadhaa tangu kuzinduliwa kwa kampeni  ya WAJIFTISHE GIFTI JUU YA GIFTI inayoendeshwa  na Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania, Bwana Jeremia Shoo mkazi wa Kilimanjaro ameibuka mshindi wa pikipiki aina ya Boxer kupitia KAMPENI YA TIGO "WAGIFTISHE  GIFT JUU YA GIFT" baada ya kununua simu katika duka la Tigo.


Meneja Mauzo wa Tigo, Moshi,Silas Mkuyu,akimkabidhi Jeremiah Shoo,mkaazi wa Machame,Kilimanjaro,mshindi wa piki piki,katika promosheni inanyoendelea ya wagiftishe gift juu ya gift.

Akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa pikipiki mshindi huyo ameishukuru Tigo kwa kuwajali wateja wake na kuamua kurudisha kwa wateja kupitia zawadi.

"Nilinunua simu ya Shilingi elfu 89 katika duka la Tigo  na hatimae tarehe 15 mwezi wa 12 , Nilipigiwa simu na Tigo kuwa nimeshinda pikipiki nawashukuru Tigo mmesongesha maisha yangu".

Alisema  Bwana Jeremia Shoo Mshindi wa Pikipiki.

Akimpongeza mshindi wa pikipiki hiyo pamoja na washindi waliojishindia simu janja Meneja wa Mauzo  Tigo Kilimanjaro, Bwana Silas Mkuyu amesema katika mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidijitali nchini, kampuni ya Tigo imewahakikishia wateja wake kuwa kila mtu anapata nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu zaidi kwa kila ununuzi wa simu za kisasa za ITEL T20 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote, hivyo akawaomba wateja waendelee kununua simu za ITEL T20 na simu nyingine kutoka maduka ya Tigo nchini kote ili kuingia kwenye droo ya kupata nafasi ya kujishindia moja ya pikipiki  5 zikiwemo simu janja zinawaniwa katika promosheni hiyo.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: