Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu amesema ameongeza suala la uendelezaji Miji na Vijiji katika vipaumbele vyake wakati anapoitumikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI.


Waziri Ummy aliyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba baina ya  Wizara ya Fedha na Mipango, na Ofisi ya Rais TAMISEMI,  Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na halmashauri zinazotekeleza mradi huo.


" Nilipohamishiwa Wizara hii nilikuwa na vipaumbele vyangu kama vinne hivi ambavyo ni huduma za Afyamsingi, usimamizi wa Elimumsingi, kuwawezesha wananchi kiuchumi na miundombinu ya TARURA lakini sasa naongeza na hili suala la uendelezaji Miji na Vijiji."


"Nimegundua ni suala muhimu sana, tusipodhibiti ukuaji wa Miji na Vijiji vyetu hata hivi tunavyovifanya havitaleta tija iliyokusudiwa, tunajenga shule au hospitali kwenye maeneo ambayo hayajapangwa tunakuwa na miji ambayo si salama kwetu na kwa vizazi vijavyo.'


Mhe Ummy aliwataka maafisa mipango miji kujipanga kutekeleza kipaumbele hicho.


" Huwezi kuwa afisa mipango miji afu eneo lako halijapangwa, mji unakua kiholela holela tu na wewe upo, mkafanyie  kazi ya kudhibiti ukuaji wa miji kiholela  na mkatilie mkazo kwenye ile miji inayochipukia."


“Katika kuimarisha hili ntarudisha Idara ya Uendelezaji Miji na Vijijini kwenye Halmashauri ili waweze kusimamia na kutekeleza kazi hii kwa ufanisi, miji lazima ipangwe na iwe salama wakati wote."


 Awamu ya kwanza  ya mgao wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi umezihusisha halmashauri 55.

Share To:

Post A Comment: