Kamishna wa Tiba na Kinga Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Dkt.Peter Mfisi akizungumza katika nyumba za utoaji huduma kwa waraibu (Sober house) ya Free at last iliyopo Mkoani Morogoro mara baada ya waandiishi wa habari za mitandao ya kijamii kufika katika eneo hilo. Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya Bw.Abeli Leonald akizungumza katika nyumba za utoaji huduma kwa waraibu (Sober house) ya Free at last iliyopo Mkoani Morogoro mara baada ya waandiishi wa habari za mitandao ya kijamii kufika katika eneo hilo.

Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya Bw.Hussein Abdallah katika nyumba za utoaji huduma kwa waraibu (Sober house) ya Free at last iliyopo Mkoani Morogoro mara baada ya waandiishi wa habari za mitandao ya kijamii kufika katika eneo hilo.

********************************

NA EMMANUEL MBATILO, MOROGORO

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) wapo katika mpango wa kutengeneza miundombinu rafiki yya ajira kwa waraibu ambao wanatoka katika matibabu ili wasiweze kupata ushawishi wa kurudia matumizi yya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika nyumba za utoaji huduma kwa waraibu (Sober house) ya Free at last iliyopo Mkoani Morogoro Kamishna wa Tiba na Kinga Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya Dkt.Peter Mfisi amesema kumekuwa na baadhi ya waraibu wamekuwa wakirudia kutumia dawa za kulevya kutokana na mazingira ambayo wanakutana nayo pindi wanapotoka kupata matibabu.

Amesema watakaa na Wizara kuona ni namna gani wanaweza kutatua changamoto wanayokutana nayo waraibu ambao wameshapata matibabu hasa kuona nini wafanye ili wakishatoka katika matibabu iwe rahisi kupata ajira ambayo iatweza kumsaidia kujikimu kimaisha na kuondokana na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa upande wa waraibu wanaopata matibabu katika kituo cha Free at Last wamesema chanzo kikubwa ambacho kinawafanya waraibu wa dawa za kulevya kujikuta wanaendelea kutumia dawa hizo pasipokupata msaada ni kutokana na jamii na marafiki waliowazunguka.

Mmoja wa waraibu hao Bw.Hussein Abdallah amesema amejikuta akiingia kwenye utumiaji wa dawa za kulevya kutokana na changamoto za maisha zilizompelekea kupata marafiki ambao walimshawishi na kuingia kwenye janga hilo.

"Kipindi ambacho nilikumbwa na matatizo mara baada ya kuondokewa na wazazi wangu ndipo nikajikuta nashawishika kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya". Amesema

Aidha amesema uwepo wa Sober house umekuwa msaada mkubwa kwa waraibu wa dawa za kulevya kwani imesaidia kupungua kwa waraibu nchini kwa maana wengi wao wamekuwa wakijiunga na sehemu ya utoaji huduma na kuweza kupona kabisa.

"Siku za mwanzo baada ya kupewa hapa nilikuwa napatwa maumivu makali sana kwasababu ya arosto lakini wenzangu walinipa moyo na kunipa matumaini ya kuwa nataka vizuri, lakini na siku kadhaa kweli mwili ukaadha kuzoea kwa maana mwanzo nilivyokuwa nyumbani sikuweza kukaa hata siku moja sijatumia dawa". Amesema

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: