Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Prof Abel Makubi, ametoa onyo  kwa Mganga Mfawidhi , Mganga Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Hospitali  ya Mkoa wa Shinyanga na kuwataka wajitathimini kwa miezi sita. 


Prof Makubi ametoa onyo hilo baada ya kukerwa na kitendo cha watendahi wa hospitali hiyo kukosa kasi ya uwajibikaji na kuchukulia mzaha suala la miradi ya fedha za IMF ambazo zinatakiwa kutumika kabla ya Juni,2022.


Katika ziara hiyo Katibu Mkuu amekuta watendahi hao bado hawajaanza mchakato wa kupata mkandarasi wa ujenzi wa jengo la ICU na dharura(EMD) ndani ya siku saba kama walivyokuwa waliopewa na Wizara ya Afya


Hivi karibuni Prof. Makubi alikutana na Watalaamu waa vifaa tiba na Ujenzi, Wakurugenzi wa Taasisi za Afya pamoja , Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa na kuwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa fedha hizo za IMF ndani ya miezi sita na kuwapa maagizo viongozi hao wanaporudi vituo vyao vya kazi kuanza mara moja utekelezaji wa kazi hiyo kwa kutumia Single source kupitia wazabuni waliokwisha fanya nao kazi ili kukamilisha haraka ujenzi na ununuzi wa vifaa

Share To:

Post A Comment: