Wednesday, 24 November 2021

MAHAWANGA AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KUTANGAZA UTALII.

 


Na, Mwandishi wetu.


Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikoba cha Women of Hope Alive Mh. Mahawanga Janeth ameungana na wanakikoba wenzake katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza utalii na vivutio mbalimbali vinavyopatikana Tanzania.


Katika kumuunga mkono Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kupitia dhamira yake ya kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana Tanzania  ili kuweza kuvutia watalii nchini ambapo Mhe Mahawanga kwa kushirikiana na wanavikoba wenzake wameweza kutembelea Mbuga ya Ngorongoro na Serengeti kwa ajili ya kujionea uzuri wa mandhari ya mbuga hizo na wanyamapori wanaopatikana hapo.


Mhe Mahawanga amefurahi kuona mazingira yalivyo mazuri na kusisitiza watanzania kutoka maeneo mbalimbali kuwa na utaratibu wa kutembelea Mbuga zetu za ndani na vivutio mbalimbali lakini pia kuwajengea utaratibu mzuri watoto kuweza kufika maana nao wanaweza kuwa mabalozi wazuri kwa sasa na hata baadae katika kulitangaza Taifa letu kwenye nyanja ya utalii na kuwavutia watu kutoka Mataifa mbalimbali kuweza kutembelea Tanzania ili kuweza kukuza uchumi wa Taifa letu kupitia sekta ya Utalii.


Aidha Mhe. Mahawanga amempongeza sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuhakikisha anaitangaza vyema Tanzania na ubunifu wake katika kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa ili kuweza kuendelea kuwapatia maendeleo watanzania lakini pia ameahidi kuendelea kuwa sambamba naye kwenye kila nyanja ili kuhakikisha mpaka kufika 2025 Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa vyema.

No comments:

Post a Comment