Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akifungua mkutano wa pili wa Kilimo Hai unaofanyika Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa TOAM,Dkt. Mwatima Juma akitoa neno  la ukaribisho kwa wajumbe na waalikwa wa mkutano huo.

Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na Mifugo  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Soud Hassan akitoa salamu za Zanzibar katika matumizi ya Kilimo Hai.

Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.


Mkutano ukiendelea.
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.

Mkutano ukiendelea,
Wadau wa Kilimo Hai kutoka mikoa yote ya Tanzania nan je ya Tanzania wakifuatilia mawasilisho na ufunguzi wa mkutano huo.


Na Calvin Gwabara - Dodoma


NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe  amewaahidi wadau wa Kilimo Hai nchini kuwa anakwenda kuanzisha Kitengo maalumu kwenye Wizara hiyo badala ya dawati lililopo sasa ili kuongeza msukumo utakaosaidia kukua kwa Kilimo hai ili kuchangia kuleta tija kwa Taifa tofauti na ilivyo sasa.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizfungua Kongamano la pili la kitaifa la Kilimo hai lililowakutanisha wadau wote kutoka ndani na nje ya Tanzania likijumuisha Wizara ya Kilimo,Mbalozi wa nchi mbalimbali,Wakulima wa Kilimo hai na wasndikaji,Mashirika ya Kimataifa,Sekta binafsi,Taasisi mbalimbali za Utafiti linalofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.

“Najua kuwa kwa sasa pale wizarani tunalo dawati linaloshughulikia masuala mbalimbali ya kilimo Hai lakini kwa kutambua umuhimu wa kilimo hiki nawaahidi kuwa nakwenda kuanzisha Kitengo maalumu na sio dawati tena ambalo nguvu yake inaonekana sio kubwa na ninamini kupitia kitengo hiki kitasaidia kuweza kufikia malengo tnayoyakusudia”Alisema Mhe. Bashe.

Naibu Waziri huyo wa Kilimo amesema duniani kwa sasa watu wamekuwa wanzingatia sana swala la afya kutokana na vyakula wanavyokula lakini pia mazao yatokanayo na kilimo Hai yanabei nzuri kuliko yae mengine yasiyo ya kilimo hai hivyo kama wizara lazima ihamasishe na kuhimiza ukuaji wa Kilimo hai Nchini.

Bashe amesema pamoja na jitihada hizo ambazo Wizara yake inakwenda kuzichukua lakini pia kwa kushirikiana na wadau hao amedhamiria kuanzisha benki ya mbegu za asili nchini ambayo itakuwa na kila aina ya mbegu nzuri ambazo wazee wamekuwa wakizutumia kwa miaka mingi ambazo zitasafishwa vizuri ili ziweze kurudishwa mashambani.

 “Namuagiza mkurugenzi wa TARI nchini kama anavyohangaika kufanya tafiti za mbegu,mbolea na madawa sasa nataka awe na kitengo maalumu cha utafiti ambacho kitakuwa kinashughulika na maswala ya kilimo hai nchini kwa upana wake” aliagiza Bashe.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa TOAM,Dkt. Mwatima Juma alisema wakati sasa hivi kwenye kongamano hili hawazungumzii tena kuwa na kilimo hai bali wanazungumzia sasa nini kifanyike maana kuendelea na malumbano ya kufaa kwa mbolea na chumvichumvi na kutofaa au kuzungumzia dawah ii na ile ni jambo ambalo halikipeleki mbele kilimo hai nchini .

“Sasa hivi kote duniani imeshafahamika kwamba matatizo ya tabia nchi,matatizo ya kiuchumi,matatizo ya ajira yote yanatokana na mfumo usiofaa wa kupeleka mbele swala zima la kilimo hai kwahiyo tujaribu kuona ni namna gani na kuweka mkakati wa namna ya kuweka mfumo mwingine” alisisitiza Dkt. Mwatima.

Aliongeza Hivi sasa mkutano mzima utasikia mamswala ya tumefanikiwa wapi, nini kifanyike kupanuka zaidi kwa sababu kuna swala zima la utafiti,swala zima la Siasa ambayo yote yanatakiwa yaende sambamba ili kuona mambo ya kilimo endelevu na kilimo hai kinapofika.

“Sababu kubwa ya mimi binafsi ya kutaka tuelekee huko ni sababu ya kiafya kwani afya zetu zinaharibika sana kutokana na mfumo wa uzalishaji ambao umeharibika kwahiyo tunauchimbua kutoka kule ili tuweze kurekebisha maswala ya afya ili kupunguza matumizi ya rasilimali zetu kwenye matibabu, Tuna swala la mazingira,tuna swala la mabadiliko ya tabia nchi pamoja na swala la uchumi wa nchi,swala la kupatikana soko kwa mazao yetu,kuongeza thamani ya amzao yetu ambayo hapo utaona kuna kuongeza ajira kwa vijana” alibanisha Dkt. Mwatima.

Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na Mifugo  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Soud Hassan alisema hivi sasa karibia asilimia 60 ya mazao ya Zanzibar ni Kilimo Hai maana walikuwa wakilima hivyo kwa muda mrefu bila kutambua kuwa ni kilimo Hai.

“Kama mnavyojua kuwa Zazibar tunalima sana viungo na kinawaingizia wakulima wetu fedha nyingi sana na kusaidia katika uchumi wao na Serikali lakini lazima tuseme ukweli kuwa kilimo Hai wafadhili wakubwa ni watu kutoka nje lakini niwahakikishie kuwa nitakaporudi Zanzibar wakati wa bajeti naiweka kilimo hai kwenye bajeti hiyo kwa lengo la kuendeleza kilimo hiki” alisisitiza Hassan.

Kongamano hilo la pili la Kilimo Hai linafanyika jijini Dodoma likiwa na kauli mbiu isemayo Kuchochea kilimo hai kwa mfumo endelevu ya Chakula.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: