Na Rhoda Simba Dodoma.


WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto imekutana na sekta binafsi  na mashirika ya kidini kujadili fursa ya uwekezaji katika sekta ya Afya hasa katika masuala ya vifaa tiba na viwanda vya madawa.


Akizungumza jijini hapa Katibu Mkuu Wizara ya  Afya Maendeleo ya  Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Profesa Abeli Makubi amesema kuwa licha ya kuwa Wizara inashughulika na masuala ya tiba lakini pia sekta hiyo  ni eneo muhimu  katika uwekezaji  hivyo wamekutana na Wadau hao  kujadili jinsi gani wanaweza kuwekeza zaidi katika sekta ya afya Kwa pamoja  kuleta maendeleo katika masuala  ya tiba

 .

"Watanzania wafanyabishara  na wawekezaji binafsi bado mna fursa nyingi ya kuwekeza kwenye sekta ya afya kuliko kuiachia Serikali  peke ake, pia sasa hivi  tumeanza kutengeneza chanjo yetu dhidi ya uviko 19 kwa kushirikiana na sekta na tupo makini kwenye hili endapo tutafanikiwa kwenye chanjo tutakua tumefanikiwa kwenye sekta binafsi "amesema Makubi


Aidha katibu mkuu huyo ameongeza kuwa serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi kwani imekuwa ikisaidia serikali katika  Kuhamasisha wananchi kuendelea kujikinga na Uviko 19  hasa katika suala la chanjo ya Uviko 19 na kuhamasisha wananchi kuendelea kujikinga  na ugonjwa huo.



 "Niwaombe sekta binafsi kuwekeza pia kwenye vyuo vya sekta ya afya kwani bado watanzania wengi wangependa kusomea masuala ya afya hapa nchini,Tanzania ina maeneo  mazuri pia ni mahala salama kwa kuwekeza kwahiyo ni fursa kubwa kwa sekta binafs kuwekeza  hususan kwenye  sekta ya afya "


 Nae dokta Gina fransis makwabe  mwenyekiti wa Chama Cha hospitali na vituo binafsi Tanzania, ameishukuru wizara kuitisha mkutano huo na kuonesha  juhudi kuwa Wizara inashirikiana vizuri na sekta binafsi  huku akibainisha kuwa Sekta binafsi zimeshiriki Kwa kiasi kikubwa katika uwekezaji kwenye masuala ya Afya nchini  hasa katika vifaa tiba na viwanda.

 

Hata hivyo kwa upande wake Sachi katwaza mwenyekiti wa Tanzania asosiation of famercitical industry, waingizaji wa Dawa na vifaaa tiba nchini ameiomba Serikali kuangalia sheria upya hasa ya ulipaji wa VAT Kwa baadhi ya vifaaa tiba  vinapowasili bandari na kubainisha kuwa    kupingana Kwa TIC na TRA kunachangia pia wao kuwa na vikwazo vingi.

Share To:

Post A Comment: