*****************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji , Mhe. Geoffrey Mwambe, leo tarehe 16 Oktoba, 2021, amekagua shughuli za uwekezaji katika Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha Mbolea asilia cha ITRACOM FERTILIZERS LIMITED, kinachojengwa katika eneo la Nala, jijini Dodoma.



Mradi huo ni miongoni mwa miradi yenye hadhi ya uwekezaji maaluum, ukiwa na mtaji wa Dola za Marekani milioni 180 na unatarajiwa kuzalisha ajira 3000. Aidha, mradi huo utasaidia kuingiza fedha za kigeni, kipato kwa wananchi na mapato ya serikali kupitia kodi



Katika ziara hiyo Mhe. Mwambe ameabatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka pamoja na Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: