Sunday, 17 October 2021

TANZANIA TOP MODEL YARUDI KWA KISHINDO


Mkurugenzi wa Kampuni ya Pakawear Gymkhana Majaliwa ambayo inajuhusisha na ubunifu wa Mavazi pamoja na Wanamitindo kwa ujumla akizungumza ujio wa Shindano la Tanzania top Model ambapo Mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha Milioni 5
Mkufunzi wa Wanamitindo wa Shindano la Tanzania top Model kwa mwaka huu Marry Chizi akifafanua zaidi kwa jinsi gani tasnia ya Urembo ilivyokua mojawapo ya fursa kwa wasichana

Afisa Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Selemani Khalifa akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kutangazwa rasmi kurudi kwa Shindano la Tanzania top Model ambapo amewataka Wasichana kuona jukwaa Hilo ni Mojawapo ya kupata fursa mbalimbali ya kujiingizia kipato

 

 

 

SHINDANO la kumtafuta Tanzania Top Model linatarajia kufanyika Machi mwakani Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendeleza na kuinua vipaji vya wasichana nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Paka Wear Company ambao ndiyo waandaji wa shindano hilo, Gymkhana Majaliwa alisema tukio hilo la mavazi ni tukio la kwanza kuanzishwa hapa nchini ambalo litatangaza vivutio vya utalii na vipaji vya wasichana.

Majaliwa alieleza kuwa shindano hilo litashirikisha wasichana wote waliopo nchini ili kupata muwakilishi ambaye ataipeperusha bendera ya Taifa katika mashindano ya Afrika.

"Shindano hili limerudi kwa mara nyingi baada ya kusimama kwa muda wa miaka saba tangu lianze kuanzishwa, pia tunaunga juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza vipaji vya wasichana nchini alisema Majaliwa.

Mratibu wa shindano, Adili Kigoda aliongezea shindano la mwaka huu litashirikisha wabunifu wachanga 22 kwa ajili ya kutangaza mavazi yao.

Kigoda amesema shindano hilo litakuwa katika hatua ya ngazi ya robo fainali, nusu fainali na fainali.

Hatua hizi za ngazi zitafanyika robo fainali itafanyika Unguja Januari, nusu fainali itafanyika Dodoma huku Fainali itafanyika Dar es Salaam, pia mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh. milioni tano, pili milioni mbili na watatu milioni moja " amesema Kigoda.

Kwa upande wake Afisa Sanaa wa  Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Selemani Khalifa ametoa wito kwa wasichana kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo ili kutimiza ndoto zao.

Khalifa alieleza kuwa BASATA limetoa baraka zote kwa shindano hilo na kuwa nao bega kwa bega katika kukuza na kudumisha mitindo nchini

 

No comments:

Post a Comment