Hayo yamesemwa na Waziri Jafo katika Mkutano wa Uzinduzi wa "Middle East Green Initiatives" uliofanyika mjini Riyadh na kuhudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali na mashirika ya kimataifa. Mkutano huo ulioandaliwa na Serikali ya Saudi Arabia na uliongozwa na Mwana Mfalme na Makamu Waziri Mkuu wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman.


Tanzania imejipanga kutekeleza uchumi wa kijani kwa kuzingayia uhifadhi wa mazingira katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo matumizi ya nishati jadidifu kwa lengo la kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kama vile Mradi wa umeme wa Maji wa Mwalimu Nyerere. Alisema Jafo.


Kwa upande wake Mwana Mfalme Mohammed Bin Salman alisema Saudi Arabia na Mataifa ya Mashariku ya Kati yameanzisha Mpango wa "Muddle East Green Initiative" kwa lengo la kushirikiana na mataifa mbalimbali katika kukuza uchumi wa kijani na kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la kujenga uchumi endelevu.

Share To:

Post A Comment: