Saturday, 23 October 2021

SPIKA WA BUNGE JOAB NDUGAI AZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUTORUHUSU MIGOGORO NA MIGONGANO ILI KUFANIKISHA LENGO Na Rhoda Simba,Dodoma.


SPIKA wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema mbali na asasi za kiraia kutoa mchango mkubwa katika kujenga nchi wanatakiwa kutoruhusu migogoro na migongano ndani ya asasi zao  ili kufanikisha malengo au azma walizo jiwekea. Spika Ndugai ameyasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya asasi za kiraia Azaki  yanayofanyika Jijini Dodoma ambapo amesema ni wakati wa asasi hizo kijitathimini na kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria zinazowaongoza


Jenipher Kato ni muakilishi wa asasi ya Wote sawa inayojishughulisha na Utoaji Elimu na kutetea wafanyakazi wa majumbani amesema kuwa katika wiki ya asasi za kiraia wanatumia kuelimisha jamii kuhusu wafanyakazi wa majumbani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kuwapa wafanyakazi wa ndani mikataba.Wiki ya asasi za kiraia inafanyika Jijini Dodoma ambapo asasi mbalimbali zinapata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yahusuyo asasi hizo pamoja na kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii.

No comments:

Post a Comment