Monday, 18 October 2021

RAIS SAMIA AWATOA HOFU WAWEKEZAJI KIWANDA CHA NYAMA LONGIDO MKOANI ARUSHA"HADI DECEMBER 5,2021 MAJI YAWE YAMEFIKA".

        Na Lucas Myovela_ Longido Arusha.

Rais wa Jamuhuri ya Muungqno wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda kikubwa nchini cha kuchakata nyama cha Eliya Food Overseas Ltd, kilichopo Wilayani Longido Mkoa Arusha.

Kiwanda hicho kimeghalimu fedha za kitanzani zenye thamani ya Shilingi Bilioni 17, Mbali na kukamilika kwa kiwanda hicho Rais samia ameahidi  kumaliza changamoto  ya Maji inayokikabili kiwanda hicho ifikapo Mwezi Disemba mwaka huu 2021. 


Akiongea katika uzinduzi huo Rais Samia amewapongeza wawekezaji hao kwa kufanya uwekezaji Mkubwa Nchini na kusema ni fursa Kwa wafugaji wa Wilaya ya Longido na Mkoa wa Arusha kwa ujumla ambapo wafugaji wataweza kuuza mifugo yao.

Rais Samia aliahidi kutatua  changamoto zingine katika kiwanda hicho ,ikiwemo upatikanaji wa malighafi ya Nyama,Masoko ya Ngozi ,pamoja na kuwapatia elimu wananchi kuacha kuweka alama kwa kuchoma ngozi za mifugo jambo linalopunguza thamani ya ngozi.

"Tumezichukua changamoto hizo ila suala la maji nataka pindi ifikapo desemba 5 mwaka huu yawe yanapatikana kiwandani hapo kwa uhakika viongozi wa Mkoa na wilaya simamieni hilo, Kiwanda hiki kitakuwa kikisafirisha nyama nje ya Nchi hivyo hivi sasa soko la mifugo ni la uhakika kwa wafugaji". Alisema Rais Samia.

Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho, lrfhan Virjee alisema   kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata tani 20 za nyama ya  ng'ombe sawa na Ng'ombe 500 kwa siku na tani 20 za nyama ya  mbuzi na kondoo,Sawa na mbuzi 4000.

"Kwa sasa kiwanda hiki kinafanya kazi kwa asilimia 30  ya uwezo wa kuchinja na kuchakata nyama kwa mifugo ya Mbuzi na kondoo na asilimia 10 kwa mifugo ya ng'ombe, Vilevile Mhe, Rais Lengo la kiwanda hiki ni kufikia uzalishaji wa asilimia 80 kufikia mwishoni mwa mwaka 2021  na  kukuza masoko mapya ya bidhaa zetu ndani na Nje ya Nchi". Alisema Irfahan.

Aidha aliongeza kwa kueleza kwamba mpaka sasa kiwanda hicho kimeshatoa ajira 150 za moja kwa moja kwa Watanzania wakiwemo madaktari  watatu wa wanyama kutoka Serikalini wanaofanya kazi za ukaguzi wa Afya na ubora wa mifugo kiwandani hapo.

Virjee alieleza baadhi ya changamoto zinazo wakabili kuwa ni pamoja na kuiomba Serikali kusaidia upatikanaji wa Ng'ombe wa bei nafuu kwa kuruhusiwa kununua mifugo kutoka moja kwa moja kwa wafugaji na hivyo kusaidia kuingia kwenye soko la ndani kwa bei nafuu.

Alisema kwa sasa wanauza  Nyama katika masoko ya nchi za uarabuni ,Oman,Qatar,Kuweit,Bahrain ,Falme Za kiarabu(UAE) na Kenya.

Hata hivyo alimwomba Rais Samia kuharakisha mazungumzo na nchi ya China na DRC CONGO ili kufikia makubaliano ya ubora wa Nyama .

Kwa upande wake waziri wa viwanda Profesa Kitila Mkumbo alisema kiwanda hicho kwa Sasa ni kati ya viwanda vikubwa 618 vya kusindika Nyama hapa nchini na kwamba kiwanda hicho ni cha kwanza kwa ukubwa kati ya viwanda 10 vya kusindika Nyama nchini.


No comments:

Post a Comment