Saturday, 16 October 2021

MSIWABAGUE WATOTO WA KIUME; REPSSI TANZANIA

Mkurugenzi Mkazi wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala akizungumza  kwenye Jukwaa la Kimataifa la Msaada wa Kisaikolojia (PSS FORUM) linalofanyika kwa njia ya mtandao, likiunganisha nchi 13 za Afrika ikiwemo Tanzania. 

Mwenyekiti wa Bodi ya REPPSI, Jeanne Ndyetabura akizungumza na wanahabari wakati Jukwaa la Msaada wa kisaikolojia likiendelea.

Watendaji wa REPSSI Tanzania wakielekezana Jambo wakati wa Jukwaa la Msaada wa kisaikolojia jijini Dar es Salaam.

Wadau wakifuatilia mada.


Tumaini Godwin, Dar es Salaam.


WADAU zikiwemo taasisi za serikali na zisizo za kiserikali zinazofanya kazi za watoto na vijana zimetakiwa kutowabagua badala yake, ziweke nguvu katika kuwasaidia watoto wa kiume kama ambavyo wanawasaidia wakike.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Kimataifa linalojihusisha na masuala ya malezi na msaada wa kisaikolojia  kwa watoto la  Regional Psychosocial Support Initiative (REPSSI) Jeanne Ndyetabura amesema ikiwa watoto wa kike watasaidiwa huku wakiume wakiendelea kuchwa wasitegemee matokeo wanayotarajia kupata.

Nyetabura alikuwa akizungumza  wakati akichangia mada kwenye Jukwaa la Kimataifa la Msaada wa Kisaikolojia (PSS FORUM) linalofanyika kwa njia ya mtandao, likiunganisha nchi 13 za Afrika ikiwemo Tanzania. 

“Watoto wa kiume mnamwachia nani? Hivi mnadhani watoto wote wa kike wanaopewa mafunzo wanaweza kuruka vihunzi vya watoto wa kiume ambao hawajasaidiwa?” alisema Ndyetabura.

Alisema kukosa taarifa sahihi kuhusu makuzi yao na watu wa kutatua changamoto zao kumewafanya watoto wa kiume watafute sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo ni hatari.

Awali Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Darius Kaijongo alisisitiza suala la malezi ya watoto kwa usawa.

Mkurugenzi Mkazi wa REPSSI Tanzania, Edwick Mapalala amesema Jukwaa la Kimataifa la Msaada wa Kisaikolojia linalenga kujadili changamoto za watoto na kuandaa mikakati ya namna ya kuziondoa ikiwemo masuala ya kisaikolojilia.

No comments:

Post a Comment