Tuesday, 12 October 2021

MSIKITI WAZINDUA MAKTABA KUSAIDIA VIJANA KUTOKWENDA NJE YA NCHI KUSOMA.

Na Lucas Myovela_Arusha.

Msikiti wa Hidaya uliopo eneo la Olmatejo kata ya Sakina, katika jiji la Arusha, umezindua Maktaba ya kisasa ya vitabu vya dini na vya elimu ya kawaida,kwa wananchi wa dini zote  ili kusaidia vijana ambao wanataka kujiendelea kielimu kujisomea,badala ya kwenda nje ya nchi kusaka elimu.

Maktaba hiyo, imezinduliwa juzi  sambamba na uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa msikiti mpya wa ghorofa nne ambao unatarajiwa kugharimu sh 2.2 bilioni.

 
maktaba hiyo ambayo itasaidia vijana wengi kusoma badala ya kutumia muda wao katika mambo ambayo sio ya msingi.

Sheikh Mkuu wa msikiti huo,Sheikh Omar bin Said  Jori alisema uzinduzi wa Maktaba hiyo na ramani ya ujenzi wa msikini wa  ghorofa nne ni sehemu yamaadhimisho ya siku ya Hidaya ambayo ni mwaka wanne sasa kuadhimishwa.

Sheikh Omari alisema vitabu pamoja ujenzi wa eneo la maktaba hiyo umegharimu zaidi ya sh 7 milioni  huku msikini utakajengwa ambao utakuwana ghorofa nne utagharimu zaidi ya sh 2 bilioni.

Sheikh Omar Kilichowasukuma kufungua maktaba hiyo ni kurejea maagizo ya mwenyezimungu kuwataka watu kusoma na sasa vijana  ambao walikuwa wakilazimika kusafiri hadi  nje yanchi kutafuta elimu wanaweza kusoma nchini.

"kufungua maktabahii ni kurejea maagizo ya  Mwenyezimungu yakutaka watu kusoma  hivyo, maktaba hiyo itatumiwa na watu wa dini zote kujisomea"alisema 

Hata hivyo, Sheikh Omar aliomba wahisani kuendelea kujitokeza kusaidia mradi wa ujenzi wa msikini huo, ambao pia utakuwa na shule ya watoto wadogo ili kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri.

Akizungumzia mradi huo,katika uzinduzi huo, diwani wa kata ya Sakina, Vincent Wilson maarufu kama Fadhili, alisema uzinduzi wa maktaba hiyo ni faraja katika kata yake kwani, sasa utaondoa tatizo la vijana kukaa mitaani bila kazi.

"lakini pia tunapongeza masjidi Hidaya kwa kuja na mradi wa ujenzi wa msikiti na shule hii itasaidia watoto kusoma kwani katika kata hii hatuna shule"alisema

Wakizungumza na mwananchi baadhi ya wakazi wa Sakina, walieleza kuzinduliwa kwa maktaba hiyo ni fursa kwao kujiendeleza kusoma kwani awali kulikuwa hakuna vitabu vingi vya dini katikajiji la Arusha.

Shaaban Juma alisema maktaba hiyo ina juzuuzote za quraani, vitabu vya hadithi,Sunna na maelekezo mbali mbali ya dini ambavyo sio rahisi kuvipata katika maeneo mengine.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment