Kamishna wa Madini Nchini Dkt. Abdul Rahmani  Shaban Mwanga kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa amefanya ziara ya kikazi Kituo cha Jemolojia Tanzania  (TGC) na kukutana na timu ya Menejimenti ya Kituo hicho huku akielezea madhumuni ya ziara hiyo ikiwa ni kujitambulisha.

Dkt.Mwanga amekipongeza kituo hicho kwa kuendelea kutoa mafunzo ya uongezeaji thamani madini nchini na kuhamasisha watanzania kuendelea kupeleka wanafunzi kujiunga na kituo hicho.

Sambamba na hilo Dkt. Mwanga ameagiza uongozi wa Kituo hicho kuongeza juhudi katika kukifanya Kituo hicho kuzidi kutambulika Kimataifa na kuvutia wateja na wadau wa sekta ya madini kutoka ndani na nje ya nchi.

Pia amekitaka Kituo cha Jemolojia Nchini (TGC) kuendelea kutoa huduma zinazoendana na soko la madini Duniani kama vile huduma za Kimaabara za utambuzi wa madini ya vito pamoja na bidhaa za usonara.

Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Daniel Kidesheni
amesema kuwa, Kituo hicho kinatoa huduma mbalimbali za uongezaji thamani madini kwa wadau ikiwa ni pamoja na utambuzi wa madini ya vito, usanifu madini pamoja na uchongaji wa vinyago vya miamba.

 

 

Share To:

Post A Comment: