Zaidi ya wapigakura 11,500 katika Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha wanatarajia kupiga kura katikaa uchaguzi mdogo wa mbunge wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Desemba 11,2021.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha  Leo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Dk.Jumaa Mhina amesema wapiga kura hao ni kwa mujibu wa kumbukumbu za daftari la mpiga kura la mwaka 2020.


Hata hivyo uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo William Ole Nasha kufariki dunia,Septemba 27 mwaka huu mjini Dodoma.


Amesema baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza uchaguzi huo na kupokea barua ya kuusimamia,wanaendelea na maandalizi na kuwa wananchi hao watapiga kura katika vituo 130 vilivyopo jimboni humo.


"Nawoamba vyama vya siasa waendelee na mchakato wao kwenye vyama ulioanza Oktoba 18 hadi 24,na uteuzi wa wagombea utafanyika Novemba 15 kabla ya kampeni kuanza Oktoba 16 mwaka huu hadi Desemba 10,"amesema


"Tunaomba amani,upendo na ushirikiano ili uchaguzi huu uende salama.Kuhusu waliopoteza kadi za kupiga kura tunasubiri maelekezo kutoka NEC na tutahakikisha  kila aliyekidhi vigezo atapiga kura,"

Share To:

Post A Comment: