Na Khadija Kalili, Kibaha
MKUU
wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ametoa wito kwa wanawake wa Mkoa wa
Pwani kuzithamini kazi zao mdogomdogo ambazo ndizo zinajenga
uchumi wa familia na nchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa
kunyanyuana.
"Nawasihi
wale ambao mnafanya biashara ndogo ndogo kunyanyuana kama jinsi
ambavyo serikali yetu ya awamu ya sita inavyoweka kipaumbele kwa
wanawake huku tukiwa tumepata bahati ya kuwa Rais mwanamke Samia
Suluhu Hassan kwakuwa amekuwa anazungumzia wanawake kila mahali
anapokuwa "alisema DC Msafiri.
DC
alisema hayo jana jioni alipokuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la
wanawake lilifahamika kwa jina la 'Fursa Gala' lililowakutanisha
wanawake wa kada mbalimbali kutoka katika Wilaya za Mkuranga, Kibaha,
Chalinze ,Mlandizi na Bagamoyo lililofanyika kwenye ukumbi wa Destiny
uliopo Kwa Mathias Kibaha Mkoani Pwani.
"Kama
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anavyohimiza utalii wa ndani na
sisi tutandaa wiki ya mjasiriamali Kibaha Ili tuweze kupeana fursa na
ninaamini tutaweza " alisema DC Sara.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda
amesema kuwa amevutiwa na mwitikio wa wanawake wa Mkoa wa Pwani jinsi
walivyojitokeza kwenye Kongamano hilo huku akiwaahidi kurudi na
kuwatembelea na kwakagua katika maeneo yao ya kazi huku akipanga kuwapa
elimu ya kutosha juu ya usalama wao mahali pa kazi.
"Nawasisitiza
kina mama kuwa makini katika maeneo yenu ya kazi kwani hakuna shughuli
yote ya kiuchumi ambayo haina athari ya kiusalama wa afya mfano ni kwa
watengenezaji wa batiki na sabuni na bidhaa zingine wengi hawana elimu
ya usalama wa afya zao mahala pa kazi hivyo sisi kama OSHA
tutatengeneza mpango wa kuwatembelea wajasiriamali wote tutawashauri na
kwakagua" alisema Khadija.
Naye
Mwanasaikolojia mbobevu aliyekuwa Mwezeshaji Dkt. Eli Waminian
amewataka wanawake kuwekeza fikra zao katika kujiamini kwa sababu
mwanamke ndiyo ngome kuu hapa duniani na dunia haiwezi kukamilika bila
ya kuwepo mwanamke hivyo wajiamini katika kilajambo wanalolifanya
watafanikiwa huku aliwataka wawe na fikra chanya na kutoamini katika
kushindwa.
"Mwanamke
ni sawa na ardhi na hii ni sayari yake hivyo wanawake waache tabia za
kuwa na malalamiko, pia amewataka wanawake kuwaunganisha watoto wao na
jamii kama jinsi ilivyokuwa zamani leeni watoto kwa kuwaunganisha na
jamii Ili hata kama ukifa leo mtoto wako aweze kuishi maisha bila uwepo
wako kwani hutoweza kyishi nae milele" alisema Dkt. Eli ambaye amekuwa
akiivutia jamii kutokana na mafundisho yake anayoyatoa kwa jamii katika
makongamano mbalimbali.
Kongamano
hilo limeandaliwa na Kampuni mbili ambazo ni HEROCHIC Suzana Mdonya kwa
kushirikiana na Vitenge na Tamrah Kibaha inayoongozwa na Nyamizi
Yasin.
Post A Comment: