Monday, 27 September 2021

WAZIRI BITEKO AWATAKA KUTUMIA MFUMO UUZWAJI MADINI

 


Waziri wa Madini Dotto Biteko ameagiza kutumika kwa mfumo wa ujazaji fomu katika uuzaji wa madini ya Tanzanite itakayowezesha upatikanaji wa taarifa za uuzaji madini kwa urahisi.


Biteko ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mererani,Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo amesema fomu hizo zitamuwezesha muuzaji wa madini ya Tanzanite kufanya biadhara yake kwa uhuru tofauti na ilivyokuwa mwanzo.


Pamoja na hayo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere kuweka walinzi katika eneo litakalitumika kwa ajili ya ukataji na uthamijishaji wa vito ili waweze kufanya biashara kwa uhuru zaidi ambapo amewataka wafanyabiashara  hao kujiwekea akiba na kutumia fedha kwa busara kwa faida ya vizazi vyao.


Amewataka wafanyabiashara wakubwa wa madini kufuata utaratibu wa usafirishaji madini kwa kulipa vibali kwani utaratibu uliokuwa ukitumika Mkoani Arusha ulisha hamishwa katika soko la madini Mererani

 hivyo shughuli zote zifanyikie Mererani.


"Hivi sasa tayari vibali 15 vya kusafirisha madini nje ya nchi vimeshatolewa kutokea Mererani na hii ndiyo heshima ya watu wa Mererani."Waxiri Biteko


"Kuna mambo mengi ya kurekebisha ya hapa na pale na mimi niwaambiemi tutaendelea kurekebisha ilimradi sekta yetu iende mbele."Alisisitiza Biteko


Akizungumzia suala la miundombinu ya  barabara iliyopo ndani ya ukuta kuelekea kwenye migodi Biteko ameahidi kuleta wataalam wa kupima ambapo pia amewaomba wachimbaji waliopo ambao wanamitaji mikubwa mshirikiane kwa pamoja.


"Mwenye wajibu wakutengeneza miundombinu ya ukuta ni serikali na tutaleta wataalam waipitie kisha tutafute fedha tuichonge watu wapite vizuri na msisubiri tu serikali,mkisubiri serikali mtachelewa."Waziri  Biteko


Sambamba na hayo Waziri Biteko amesema takribani asilimia 32 imetumika katika  kujenga bwawa la Mwalimu nyerere imetokana na mapato ya shilingi trioni 7 kipitia dhahabu inayosafirishwa nchini kwa mwaka ambapo asilimia 32 inatokana na wachimbaji wadogo.


Awali Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka amesema akiwasilisha ombi la ukarabati wa barabara inayoelekea kwenye migodi kwani imekuwa kilio na changamoto ya muda mrefu kwa wachimbaji hao kutokana na ubovu uliopo.


Sendeka amesema pamoja na ukwepo wa ukuta na ulinzi imara katika mdogi huo bado ipo changamoto ya ufungiwaji wa madini ambao haujatoa nafasi ya mchimbaji kuthaminisha madini yake hivyo kumlazimu kuuza madini hayo kwa gharama yoyote ambayo haitampa faida.


"Kwa ukufanya hivyo ukiritimba utaondolewa wa matajiri wachache wenye leseni za wafanyabiashara wakubwa kuuziwa madini kwa bei za nyanya."Christopher Ole Sendeka


Ameongeza kuwa biashara za ukataji na uongezaji wa thamani madini ya Tanzanite ikifanyika katika eneo la Mererani peke yake wananchi wazawa watanufaika na madini yao na kufanya mji wa Mererani uwe mji wa kitalii.

No comments:

Post a Comment